Kumbukumbu ya Dr Martin Luther King, Jr

Dkt Martin Luther King, Jr. akiwa na Mchungaji Jesse Jackson (kushoto) muda mfupi kabla ya kutoa hotuba yake ya mwisho kwa wafanyakazi wanaofanya usafi katika mji wa Memphis waliokuwa katika mgomo April 4, 1968.

Attendees are seen during a silent march and rally on the National Mall to mark the 50th anniversary of the assassination of civil rights leader Rev. Martin Luther King Jr. in Washington, U.S., April 4, 2018. REUTERS/Eric Thayer TPX IMAGES OF THE DAY - RC1328E3CB80

Watu waliohudhuria maadamano ya kimya kimya na mkusanyiko mkubwa katika eneo la National Mall kuadhimisha miaka 50 ya kuuwawa kwa kiongozi wa haki za raia Mchungaji Martin Luther King, Jr. huko Washington, Marekani Aprili 4, 2018.


Picha ilipigwa kutoka angani ikionyesha wingu la moshi lililokuwa linaendelea kusambaa kutoka katika majengo yaliyokuwa yanaunguwa upande wa kaskazini mashariki ya Washington, DC, Aprili 5, 1968.


Yolanda Renee King, mjukuu wa Martin Luther King Jr, akiongea wakati katika maandamano ya kushinikiza Uhai wetu wakiunga mkono kuwepo udhibiti wa silaha mjini Washington, Machi 24, 2018.


Watoto wa Mchungaji Martin Luther King, Jr., kutoka kushoto Dexter Scott King, the Rev. Bernice King, Martin Luther King III and Yolanda King Februari 6, 2006.


Martin Luther King III akiongea katika Kanisa la Church of God in Christ, Jumanne, April 3, 2018 huko Mji wa Memphis, Tennessee, Marekani.


Mwanamke aliyekuwa hajatambulika akilia wakati mamia ya waombolezaji wakipita kutoa heshima zao za mwisho  kwa mwili wa kiongozi wa haki za raia Martin Luther King, Jr., April 5, 1968, kabla ya kupelekwa kuzikwa huko Atlanta.


Mchungaji Martin Luther King Jr. akiwa na viongozi wengine April 3, 1968 ambao ni wanaharakati wa haki za raia siku moja kabla ya kuuwawa.

Dr Martin Luther King Jr. akiwashukuru waandamanaji katika eneo la Lincoln Memorial kwa kusikiliza hotuba yake ya "Nina ndoto" (I have a dream" ) huko Washington, Agosti 28, 1963.

Coretta Scott King, mjane wa Dr Martin Luther King, Jr., akiwa anatokwa na machozi, katika ibada ya mumewe kwenye Kanisa la dhehebu la Baptist Atlanta , April 9, 1968.

Kabla na baada ya mauaji ya Martin Luther Jr