Kukatika kwa umeme kwa muda mrefu zaidi kote nchini Kenya katika kumbukumbu za Wakenya kumebaki kuwa kitendawili leo Jumapili wakati kampuni ya umeme inayomilikiwa na serikali ikilaumu kufeli kwa kiwanda kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme kwa njia ya upepo barani Afrika ambacho kina jukumu mbadala kwa gridi ya umeme.
Baadhi ya zaidi ya watu milioni 50 wa Kenya ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu Nairobi walishuhudia umeme ukirejea karibu saa 24 baada ya hitilafu kubwa kutokea Ijumaa jioni. Ilikuwa ni aibu kwa kwa nchi hiyo ambayo ni kitovu cha uchumi Afrika Mashariki inayojitangaza kama kituo cha teknolojia katika bara hilo lakini bado ina changamoto kutokana na utawala mbaya na miundo mbinu duni.
Mamia ya watu walikwama gizani kwa saa kadhaa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenya mjini Nairobi na kusababisha katika hatua ya nadra Waziri wa serikali kuomba msamaha kwa umma, katika nchi ambayo utalii ni sehemu muhimu ya uchumi. Hali hii haitatokea tena Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen, alisema.