Korea Kusini ipo katika utayari baada ya shambulizi la Hamas, Israel

Korea Kusini, ipo kwenye tahadhari kubwa, ikitathimini jinsi mzozo unaoendelea mashariki ya kati unaweza kuathiri usalama wa taifa lake baada ya shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la kundi la Palestina, Hamas liliafanywa dhidi ya Israel.

Mshauri wa usalama wa taifa wa Korea Kusini, Cho Tae-yong, anachunguza athari zinazoweza kusababishwa na mzozo wa Hamas, na Israel, kwa usalama wa Korea Kusini, ilisema ofisi ya Rais Yoon Suk Yeol, Jumatatu.

Shambulio la Hamas dhidi ya Israel, Jumamosi, ambalo ni baya zaidi kutokea katika kipindi cha miaka 50, lilionekana kuongeza mzozo na kuwa vita kamili kwa siku zake sasa.

Jeshi la Israel limewakusanya askari wa akiba 300,000 Jumatatu wakati likiendelea na mashambulizi ya kujibu ya mashambulizi ardhini, angani na baharini ya Hamas.

Israel pia imeweka kizuizi kamili cha Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Wapalestina.