Korea kaskazini inataka vikwazo vya kimataifa kupiga marufuku usafirishaji wake wa chuma na uagizaji wa mafuta yaliyosafishwa, na mahitaji mengine kuondolewa ili kuanzisha tena mazungumzo ya nyuklia na Marekani, wabunge wa Korea kusini walisema Jumanne.
Kaskazini pia imetaka kulegezwa kwa vikwazo kwa uagizaji wake wa bidhaa za kifahari ili kuweza kuingiza pombe na bidhaa nyingine, wabunge walisema baada ya kuarifiwa na idara kuu ya upelelezi ya Korea kusini. Mkutano huo ulikuja wiki moja baada ya mataifa hayo mawili ya Korea kurejesha tena laini za simu ambazo Korea kaskazini ilisitisha mwaka mmoja uliopita.
Vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali ya Korea kaskazini havikutaja hii leo juu ya ombi lolote jipya la kuondoa vikwazo na kuanza tena mazungumzo.