Korea Kaskazini yaonya kuwa wanajeshi wake wapo tayari kukabiliana na Korea Kusini

  • VOA News

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, akikabidhi wanajeshi wake bendera ya nchi. Picha ya maktaba.

Korea Kaskazini Jumapili imesema kuwa wanajeshi wake wa msitari wa mbele  wako tayari kufanya mashambulizi dhidi ya Korea Kusini, na kwa hivyo kuongeza hali ya taharuki kwa hasimu wake huyo anayedaiwa kurusha droni zilizoangusha vijikaratasi kwenye mji mkuu wa Pyongyang.

Korea Kusini haijakiri wala kukanusha madai hayo, lakini ilisema kuwa ipo tayari kuadhibu Kaskazini, iwapo usalama wa watu wake utahatarishwa. Korea Kaskazini Ijumaa ilidai kuwa Korea Kusini ilirusha droni zilizoangusha vijikaratasi vyenye propaganda mjini Pyongyang, mara 3 mwezi huu, huku akiahidi kujibu vikali iwapo hilo litafanyika tena.

Kupitia taarifa kwenye chombo cha habari cha serikali Jumapili, wizara ya Ulinzi ya Korea Kaskazini imesema kuwa jeshi limetoa amri ya kupelekwa kwa silaha pamoja na wanajeshi karibu na mpaka wa Korea Kusini , wakiwa tayari kuanza mashambulizi.

Jumapili, dada mwenye nguvu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alieleza kuwa hatua ya “ kujiangamiza” onyo kutoka wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini kwamba utawala wa Korea Kaskazini utamalizwa iwapo utadhuru raia wa Korea Kusini .

Korea Kaskazini mara kwa mara hutoa onyo za aina hiyo kila kunapokuwa na uhasama ulioongezeka kati yake na Korea Kusini au Marekani.