Kifo cha mwanafunzi wa Kimarekani, Otto Warmbier, kimezua mjadala mkubwa Jumatatu baada ya kuachiwa kutoka katika gereza la Korea Kaskazini.
Mwanafunzi huyo alifariki Jumatatu akiwa katika hali ya kudhoofika na hajitambui.
Hali yake imezua mjadala kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na serekali ya Kim Jong Un.
Mwezi Januari mwaka 2016, Warmbier alikamatwa mjini Pyongyang kwa kushutumiwa kuiba tangazo la propaganda katika hoteli.
Alihukumiwa kukaa gerezani kwa miaka 15 na kufanyishwa kazi ngumu, baadaye alianza kuumwa na kupoteza fahamu miezi 15 iliyopita ambapo hakuwahi kupata tena fahamu.
Maafisa wa Korea Kaskazini wamesema Mmarekani huyo aliyekuwa na miaka 22 wa chuo kikuu cha American alikumbwa na maradhi yanayoitwa botulism na kupewa dawa za usingizi hivyo kutojitambua.