Korea Kaskazini yaishutumu Ukraine, na Marekani kuivamia Russia

Korea Kaskazini Jumapili imeshutumu hatua ya Ukraine kuingia Russia na kuiita kuwa ni tukio la kigaidi linaloungwa mkono na Washington na mataifa ya magharibi, ikiongeza kwamba itaendelea kusimama na Russia wakati inalinda dola lake kwa mujibu wa chombo cha habari cha serikali.

Chombo hicho cha habari cha KCNA kimesema hatua ya Ukraine kusomba mbele mpaka Russia ni sehemu sera ya Marekani ya kuipinga Russia, ambayo inasukuma hali ya uwezekano wa vita vya tatu vya dunia.

Ripoti hiyo imeongeza kusema kwamba Marekani imetoa silaha kali kwa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy.

Korea Kaskazini imesema inapinga vikali shambulizi dhidi ya himaya ya Russia na utawala wa kibaraka Zelenskyy chini ya udhibiti na msaada wa Marekani na washirika wake wa magharibi na kwamba si kitendo cha kusameheka cha kigaidi.