Korea Kaskazini yafanya majaribio ya silaha mapema Ijumaa

Wakazi wa Korea kaskazini watazama jaribio la silaha .Oktoba 28,2022.

Jeshi la Korea kusini limesema kwamba Korea kaskazini Ijumaa imerusha makombora mawili ya majaribio.

Huo unaonekana kuwa mwendelezo wa majaribio ya hivi karibuni, ambayo yameongeza hali ya taharuhi kati ya taifa hilo na Marekani pamoja na washirika wake.

Kulingana na mkuu wa jeshi wa Korea kusini, Korea kaskazini imerushia silaha hizo kwenye ufukwe wake wa mashariki ulioko jimbo la Gangwon, karibu na mpaka wa Korea kusini ,mida ya mchana kwa saa za huko, bila kutoa maelezo zaidi.

Taarifa kutoka kamandi ya Marekani ya Indo Pacific imesema kwamba jaribio hilo halihatarishi maisha ya vikosi vyake wale vile vya washirika , ingawa program ya nyuklia ya Korea kaskazini inayumbisha utulivu wa kieneo.

Tangu mwanzo mwa mwaka huu, taifa hilo limefanya majaribio 46 ya silaha, yakiwa kinyume na mapendekezo ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa . Pyongyang inakisiwa kufanya jaribio jingine la silaha ya nyuklia hivi karibuni baada ya lile la 2017.