Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora ya masafa mafupi kuelekea baharini Jumapili kwa mujibu wa majirani.
Inaelezwa hiyo ni kukamilisha harakati za majaribio ikiwa ni kujibu mazoezi ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini yanayo chukuliwa kama maandalizi ya uvamizi.
Muendelezo wa majaribio ya Korea Kaskazini yanaonyesha juhudi za taifa hilo kutokata tamaa licha ya mazoezi ya Korea Kusini na Marekani ambayo ni makubwa na kipekee kufanyika baada ya miaka kadhaa.
Lakini wataalamu wengi wanasema pia ni sehemu ya madhumuni ya Korea Kaskazini kupanua uwezo wake wa silaha ili kutambuliwa ulimwenguni kama taifa la nyuklia na kuondolewa vikwazo vya kimataifa dhidi yake.
Wawakilishi wa masuala ya nyuklia kutoka Korea Kusini, Japan, na Marekani walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio hayo kwa sababu yanatishia usalama wa peninsula ya Korea.