Makombora hayo yamerushwa kutoka pwani ya Wonsan, Korea Kaskazini, asubuhi, saa tano kasoro dakika 12, kwa saa za Korea Kaskazini.
Yameanguka katika bahari kati kati ya Peninsula ya Korea na Japan.
Majeshi ya Korea Kusini, Marekani na Japan yameshutumu hatua hiyo ya Korea kaskazini na kuonya kwamba inatishia hali ya amani ya eneo hilo.
Hii ni mara ya kwanza katika muda wa siku nane, Korea Kaskazini imefyatua makombora, baada ya mwezi mzima wa kurusha makombora kadhaa yakiwemo ya masafa marefu.
Wataalam wamesema kwamba Korea kaskazini ina mipango ya kuongeza utengenezaji wa silaha za Nyuklia, kwa kiwango kinachokaribia cha mataifa ya magharibi na washindani wake.