Kombora jipya laongeza mvutano Rasi ya Korea

Wananchi wa Korea Kaskazini wakimsikiliza kiongozi wao Kim Jong Un akitoa amri kujaribio kwa kombora la balistika la Hwasong-15, Jumatano, Novemba 29, 2017

Korea Kaskazini imefanya Jumatano jaribio jipya la kombora la masafa ya mbali, ikiwa ni la kwanza tangu mwezi September.

Jaribio hilo kwa mujibu wa vyanzo vya habari katika Rasi ya Korea limeongeza hali ya mvutano wakati Pyongyang ilipotangaza kuwa hivi sasa inauwezo wa kuipiga kwa nyuklia marekani kwa silaha za nyuklia.

Kombora jipya la masafa ya mbali HWASONG- 15 la balistiki limekuwa na mafanikio katika majaribio yaliyofanywa kwa mujibu wa uamuzi wa kisiasa na kimkakati wa Chama cha Wafanyakazi wa Korea.

Tangazo hilo limetolewa mapema hivi leo Jumatano katika kituo cha televisheni cha taifa cha KRT cha Korea Kaskazini.

Kufuatia majaribio ya awali, Korea Kaskazini imedai kuwa kwa makadirio yake inauwezo sasa wa kuipiga sehemu yoyote ya marekani kwa nyuklia.

Lakini hii itakuwa ni mara ya kwanza kuweza kufanya hivyo kwa kutumia aina mpya ya kombora ambalo maafisa wa Marekani na Korea Kaskazini wamethibitisha kuwa inaweza kufika mbali zaidi kuliko yale ya siku za nyuma.