Kombe la dunia: Iran yaichapa Wales 2-0

Wachezaji wa Iran kabla ya mchezo wao na Uingereza katika uwanja wa Khalifa, Doha, Qatar, Novemba 21, 2022.

Iran Ijumaa imepata ushindi katika dakika za majeraha za nyongeza kwa kuitandika Wales mabao 2-0 katika mchuano wao katika kundi B.

Timu ya Wales ya Gareth Bale ilimaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya goli kipa wao Wayne Hennessey kupewa kadi nyekundu.

Rouzbeh Cheshmi na Ramin Rezaeian wamefunga mabao na kuipa ushindi mzuri Iran, ambayo imechukua na fasi ya pili katika kundi B nyuma ya Uingereza, ambayo itamenyana baadaye leo na Marekani.