Kombe la Dunia: Ghana yaipa matumaini ya ushindi Afrika

Your browser doesn’t support HTML5

Mwaka 2010 Ghana ilikuwa timu ya tatu barani Afrika kufikia robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia huku ikibeba matumaini ya bara hilo huko Afrika Kusini.

Walimaliza mbele ya Australia na Serbia, katika kundi lao kisha wakawashinda Wamarekani kabla ya kushindwa kwa mikwaju ya penalti baada ya utata katika mechi dhidi ya Uruguay mjini Johannesburg. Baada ya kushiriki vibaya nchini Brazil miaka minne baadae Ghana wamerejea katika hatua kubwa ya soka duniani. Sikiliza uchambuzi wa mwandishi wa VOA akiwa nchini Qatar...