Hiki ni kiwango kikubwa sana kurekodiwa katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.
Hii inahusishwa na kupanda sana kwa gharama za nyumba, umeme, maji, gesi na mafuta ya aina nyingine, ambazo zilirekodo kiwango cha juu cya mfumuko wa bei mpaka asilimia 79.
Jumanne, Ghana ilifikia mkataba wa awali huko IMF kwa kupatiwa dola bilioni 3 za kuwasaidia kupata idhini ya bodi ya shirika hilo la kimataifa la fedha kama nchi itakidhi mahitaji yote yaliyowekwa.
Makubaliano yalitarajiwa kusaidia kurejesha uthabiti wa kiuchumi wa Ghana na kuhakikisha uendelevu wa deni.