Serekali kadhaa za Afrika magharibi zinajaribu kudhibiti mlipuko wa kipindupindu, ikiwa ni pamoja na Nigeria ambapo afisa wa ngazi ya juu wa afya Alhamisi amesema kwamba mamilioni ya watu wanapewa chanjo ili kufidia mapengo makubwa ya kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Takriban watu 573 kati ya 11,640 walioambukizwa kipindupindu Nigeria, wamekufa tangu mlipuko wa sasa uanze Desemba 2022, ingawa maafisa wanakadiria idadi hiyo ambayo sasa inapungua kwa sababu ya juhudi za matibabu inaweza kuwa kubwa zaidi katika majimbo ambayo hayawezi kugundua maambukizo mengi.
Nchini Niger, watu 37 wamefariki dunia katika kesi 865 kufikia Oktoba, wakati Guinea imeripoti vifo 58 kati ya maambukizi 497 tangu kuzuka kwake mwezi Juni.
Maambukizi hayo ya bakteria yanayo samba kwa kasi yameripotiwa katika majimbo 20 kati ya 36 ya Nigeria mpaka hivi sasa.