Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge, ameshinda mbio za Marathon za London kwa mara ya tatu Jumapili.
Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti Jumapili kuwa Kipchoge ambaye ni moja wa wakimbiaji hodari alianza mbio hizo akitumia muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 27.
Kwa upande wa mwanariadha wa Uingereza Mo Farah yeye aliongoza katika hatua za awali kabla ya kupoteza mwelekeo na hivyo basi kumaliza nafasi ya tatu dakika tano nyuma ya Kipchoge.
Naye mwanariadha wa Ethiopia Tola Shura Kitata aliweza kumaliza katika nafasi ya pili akiwa nyuma kwa sekunde 33 dhidi ya Kipchoge.
Vivian Cheruiyot amepata ushindi wake wa kwanza wa London Marathon.
Vivian Cheruiyot wa Kenya alishinda kwa upande wa wanawake kwa kudhibiti muda wake uliopelekea kufanya vizuri katika mashindano hayo.