Kiongozi wa upinzani Afrika kusini anatoa wito kwa wafuasi kukipigia kura DA

John Steenhuisen, kiongozi wa chama cha upinzani cha DA nchini Afrika kusini.

Chama cha Democratic Alliance kilishika  nafasi ya pili kwa idadi ya kura katika uchaguzi uliopita wa Afrika kusini

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini ametoa wito kwa wapiga kura siku ya Jumapili, kukipigia kura chama chake kwa sababu hakitoi ahadi tupu, siku chache kabla ya uchaguzi ambao unaweza kushuhudia chama tawala cha African National Congress (ANC) kikipoteza wingi wake wa viti kwa mara ya kwanza.

Chama cha Democratic Alliance (DA) ambacho kilishika nafasi ya pili kwa idadi ya kura katika uchaguzi uliopita, kiliwasihi wafuasi wake kutumia kalamu zao kufunga mlango wa ANC, ambayo kilisema ukiigubikwa na “ukosefu wa ajira, ufisadi na utawala mbaya”, na kuandika ukurasa mpya wakati wanapopiga kura Mei 29.

Tofauti na vyama vingine vyote katika uchaguzi huu, DA haitoi ahadi juu ya kile tutakachofanya siku moja. Tunakuonyesha ushahidi wa kile ambacho tayari tunafanya leo, kiongozi wa DA John Steenhuisen aliwaambia wafuasi wake, ambao walivaa rangi za bluu za chama.

DA inayounga mkono biashara inaendesha serikali ya jimbo la Western Cape, makaazi ya mji maarufu wa utalii wa Cape Town. Kura za maoni zinabashiri ANC kupoteza wingi wake wa viti bungeni kwa mara ya kwanza, tangu Nelson Mandela alipopigiwa kura kuingia madarakani mwaka 1994 na kumaliza mwisho wa ubaguzi wa rangi.