Kiongozi wa Madagascar Andry Rajoelina ashinda  muhula wa tatu

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina (katikati) alipohudhuria kutangazwa kwa matokeo ya awali katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais wa Madagascar mjini Antananarivo, Novemba 25, 2023.

Kiongozi aliyeko madarakani wa Madagascar Andry Rajoelina alifanikiwa kushinda  muhula wa tatu baada ya tume ya uchaguzi (CENI) siku ya Jumamosi kusema kuwa amepata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa rais uliokuwa na idadi ndogo ya wapiga kura na  kususiwa na upinzani.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na CENI mwishoni mwa kujumlisha kura yalionyesha Rajoelina akipata asilimia 58.9 ya kura akifuatiwa na Siteny Randrian-asoloniaiko, mbunge aliyepata asilimia 14.4.

Mahakama Kuu ya Katiba nchini humo imepewa jukumu la kutangaza matokeo ya mwisho ndani ya siku tisa baada ya tume ya uchaguzi kutangaza matokeo ya muda.

Siku ya Ijumaa wapinzani wake walikuwa wametangaza kuwa hawatakubali matokeo.

Wakati huo huo mgombea urais wa upinzani nchini Madagascar amekata rufaa katika mahakama ya juu nchini humo akitaka kufutwa kwa matokeo ya kura yaliyotangazwa Jumamosi ambayo yalimtangaza Rais anayemaliza muda wake Andry Rajoelina kuwa mshindi katika duru ya kwanza.

Niliwasilisha maombi mawili ya kuomba kufutwa kwa kura na kutostahiki kwa Andry Rajoelina,"Siteny Randrian-asoloniaiko aliiambia AFP siku ya Jumamosi, akilaani wizi wa kura katika uchaguzi huo.