Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuzuru Russia

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akihudhuria mkutano mkuu katika Ukumbi wa Mansudae huko Pyongyang.AFP.

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA lilisema Jumatatu kwamba kiongozi wake atakutana na kuzungumza na Putin wakati wa ziara yake nchini Russia.

Kremlin na Pyongyang zilisema Jumatatu kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un atazuru Russia katika siku zijazo kwa mwaliko wa Rais Vladimir Putin.

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA lilisema Jumatatu kwamba kiongozi wake atakutana na kuzungumza na Putin wakati wa ziara yake nchini Russia.

Vyombo vya habari vya Korea Kusini viliripoti Jumatatu kwamba treni maalum inayodhaniwa kuwa imembeba Kim iliondoka Pyongyang na kwamba mkutano na Putin unaweza kufanyika kuanzia Jumanne.

Maafisa wa Korea Kusini walisema wanafuatilia kwa karibu lakini hawakuthibitisha taarifa kamili.

Serikali ina wasiwasi kuhusu uwezekano wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Russia, ambao umeibuliwa hivi karibuni.Kwa mara nyingine tena, tunaweka wazi kwamba ushirikiano baina ya nchi hizo mbili haupaswi kudhoofisha utaratibu na amani ya kimataifa katika Peninsula ya Korea alisema msemaji kutoka Wizara ya Muungano ya Korea Kusini siku ya Jumatatu.