Kiongozi wa Korea Kaskazini asema 2024 ataendeleza zaidi harakati zake

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameapa kuzindua zaidi satelaiti za ujasusi za kijeshi, kuzalisha zaidi vifaa vya nyuklia, na kuanzisha ndege zisizo na rubani za mashambulizi kwa mwaka 2024.

Amezungumza hayo akielezea utayari wa kivita ili kukabiliana na hatua za kichokozi za Marekani vimeripoti vyombo vya habari vya serekali Jumapili.

Kauli za kiongozi huyo amezitoa wakati wa mkutano wa chama cha wafanyakazi ambacho kilijiwekea malengo kwa mwaka huu mpya na kueleza kuongeza majaribo ya silaha kabla ya uchaguzi wa Novemba wa Marekani.

Waangalizi wanasema Kim anaamini katika kuongeza uwezo wa silaha za nyuklia na kumpatia fursa nyingine kubwa ya kidiplomasia na Marekani, ilia pate ahueni ya vikwazo kama rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump atarejea madarakani.