Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba "mwenyewe alitangaza kujiuzulu ili kuepusha makabiliano na madhara makubwa ya kibinadamu na mali", viongozi wa kidini na jumuiya walisema katika taarifa.
Ilifuatia makubaliano kati ya mkuu wa kikundi cha utawala wa kijeshi na kiongozi mpya aliyejitangaza, Ibrahim Traore, na viongozi wa kidini na kijamii, waliongeza
Vyanzo vya kidiplomasia vya kikanda vilisema Damiba ambaye mwenyewe alichukua mamlaka mwezi wa Januari alikimbilia katika mji mkuu wa Togo Lome siku ya Jumapili kufuatia mapinduzi ya pili katika taifa hilo lisilokuwa na utulivu la Afrika Magharibi mwaka huu.
Viongozi hao wa kidini na kijamii kwa jumla pia walisema kuwa Damiba aliweka masharti saba ya kuachia madaraka.
Haya yalijumuisha hakikisho la usalama kwake na washirika wake katika jeshi na kwamba wale wanaochukua mamlaka lazima waheshimu ahadi aliyoitoa kwa kanda ya Afrika Magharibi ya kurejea katika utawala wa kiraia ndani ya miaka miwili.