Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh auawa nchini Iran

  • VOA News

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa mjini Teheran Jumatano, kulingana na taarifa tofauti zilizotolewa na Hamas na kikosi cha ulinzi cha Iran.

Hakuna aliyedai mara moja kuhusika na mauaji hayo, lakini hapo awali Israel ilisema itamuua Haniyeh na viongozi wa Hamas baada ya shambulizi la kigaidi la Octoba 7 ndani ya Israel.

Katika taarifa yake, Hamas ilisema inaomboleza kifo cha Haniyeh, ikisema aliuawa katika “shambulizi la kikatili kwenye makazi yake mjini Teheran.”

Haniyeh alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Iran Massoud Pezekshian Jumanne.

“Mapema asubuhi hii, makazi ya Ismail Haniyeh mjini Teheran yalishambuliwa, yeye na mmoja wa walinzi wake waliuawa. Sababu ya mauaji hayo inachunguzwa na itatangazwa baadaye,” Kikosi cha Revolutionary Guards kimesema.

Televisheni ya serikali ya Iran iliripoti kuhusu kifo cha Haniyeh mapema Jumatano.