Kiongozi mkuu wa Iran, ametoa onyo Jumanne kwa mgombea pekee wa mageuzi katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo, akisema yeyote anayeamini njia zote za maendeleo zinatoka Marekani hapaswi kuungwa mkono.
Akiongea kwa mafumbo kama wanasiasa wengi wa Iran, kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei, ameonekana kukosoa moja kwa moja ugombea wa daktari wa upasuaji wa moyo Masoud Pezeshkian mwenye umri wa miaka 69, ambaye amejiweka sawa na maafisa wa utawala wa Rais wa zamani Hassan Rouhani.
Rouhani alisaidia kufikia makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015 na mataifa yenye nguvu duniani, makubaliano ambayo Pezeshkian ameyakubali kikamilifu tofauti na wapinzani wake watano wenye misimamo mikali, ambao wanataka makubaliano kamili kuhusu masharti ya Iran.
Khamenei pia ametoa wito wa watu kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Ijumaa, ambao wachambuzi wanasema wanaweza kumuunga mkono Pezeshkian.