Msumbiji inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa rais kesho jumatano ambapo mshindi anatarajiwa kuwa na wakati mgumu ofisini, kukabiliana na uchumi mbaya, hali mbaya inayosababishwa na vimbunga, ukosefu wa usalama, kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya gesi na deni kubwa la serikali.
Mgombea wa chama tawala Daniel Chapo anatarajiwa kushinda uchaguzi huo, japo kuna wagombea wengine watatu wanaotafuta kuingia madarakani baada ya rais Filipe Nyusi kuondoka.
Deni kubwa la serikali limepelekea nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika kukumbana na hali ngumu ya kifedha ambayo imeathiri miradi ya uzalishaji gesi.
Msumbizi inakabiliwa na matatizo ya kifedha kutokana na wizi wa pesa zilizokuwa zimechukuliwa kama mkopo kwa ajili ya sekta ya uvuvi.
Serikali ilishindwa kulipa pesa hizo zilizopotea.