Kimbunga Ida chapungua nguvu lakini bado hatari

Mtu mmoja akipita eneo la French Quarter ambapo paa la nyumba limeng'olewa na kimbunga Ida huko NMew Orlens Louisiana. Jumapili Agosti 2021.

Kimbunga Ida kimepungua nguvu na kuwa dharuba ya kitropiki, lakini bado inaendelea kubeba upepo wenye  nguvu huko New Orleans na maeneo  ya karibu.

Kimbunga Ida kimepungua nguvu na kuwa dharuba ya kitropiki, lakini bado inaendelea kubeba upepo wenye nguvu huko New Orleans na maeneo ya karibu. Kituo cha Kimbunga cha Kitaifa kinasema Ida imesababisha kuongezeka kwa dharuba ya hatari, upepo mkali na mafuriko kusini mashariki mwa Louisiana na kusini mwa Mississippi.

Entergy, kampuni ya umeme inayosambaza umeme huko New Orleans ilisema katika taarifa Jumapili: "Kutokana na matokeo ya kiwango cha janga la Kimbunga Ida, njia zote nane za usafirishaji zinazotoa umeme katika eneo la New Orleans kwa sasa hazifanyi kazi. Umeme hautarejeshwa jioni hii, lakini tutaendelea na kazi ya kutengeneza.

New Orleans haina umeme kabisa, kulingana na nola.com, na kumaliza shida hiyo inaweza kuchukua siku kadhaa, lakini zinaweza kuwa nyingi zaidi kwa sababu moja ya minara inayotumiwa kutoa nguvu za umeme kwa jiji hilo umeanguka katika Mto Mississippi.