Kimbunga Ian kimesababisha uharibifu mkubwa kusini magharibi mwa Florida, watu wakishindwa kuondoka nyumbani kwao kutokana na mafuriko, paa la hospitali ambapo wagonjwa walikuwa wamelazwa katika chumba cha wagonjwa walio mahtuti kiafya kuharibika, huku zaidi ya milioni 2 na nusu wakiwa bila nguvu za umeme.
Kimbunga hicho sasa kinaelekea bahari ya Atlantic ambapo kinatarajiwa kutua hii leo.
Kimbunga Ian kimetajwa kuwa mojawapo ya vimbunga vyenye nguvu sana kuwahi kupiga jimbo la Marekani la Florida na kusababisha mafuriko makubwa kwenye kisiwa hicho.
Kilikuwa na kasi ya kilomita 665 na karibu jimbo lote la Florida limeshuhudia ukali wake.
Kituo cha kutabiri vimbunga cha Marekani kimesema kwamba kimbunga Ian kimepiga Florida mapema alhamisi na kinatarajia kupata nguvu tena baadaye leo alhamisi.