Kimbunga Freddy kimepiga Msumbiji na kusababisha mvua kubwa ambayo maafisa wametaja kuwa hatari na ya kipekee.
Kimbunga Freddy kimepiga mji wa Vilanculos kwa kikiwa na upepo wa kasi ya kimolita 113 kwa saa.
Kinatarajiwa kupungua kasi kinapoelekea Afrika kusini lakini watabiri wameonya kwamba kinaweza kusababisha mvua kubwa nchini Zimbabwe, Afrika kusini, Zambia, Malawi na Botswana.
Kimbunga hicho kilikuwa kimepungua kasi kilipofika Madagascar jumanne usiku, ambapo kiliua watu wanne na kuwacha zaidi ya 16,000 bila makao.
Kilipata nguvu tena jumatano na alhamisi usiku wakati kinaelekea Msumbiji.