Kimbunga chaleta maafa India

Waokoaji walitumia boti kuwasaidia watu waliokwama ndani ya nyumba zao kusini mashariki mwa India huku kukiwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga Michaung, ambacho kilisababisha vifo vya watu 13 na kuwalazimisha maelfu ya watu kuhama.

Mvua kubwa iliyotanguliwa na kimbunga ambacho kilishambulia Jumanne katika jimbo la Andhra Pradesh, kilisababisha miti kung’oka na miundombinu kuharibiwa.

Katika jimbo la karibu la Tamil Nadu, dhoruba hiyo pia ilisababisha uharibifu mkubwa na kulazimisha kufungwa kwa uwanja wa ndege katika mji mkuu, Chennai, huku magari mengi yakisombwa na mafuriko hayo.

Waziri Mkuu wa Jimbo la Tamil Nadu M. K. Stalin aliomba dola milioni 600 kutoka kwa Waziri Mkuu Narendra Modi kusaidia kulipia juhudi za uokoaji.