Wakati wa kikao hicho kllichofanyika Slovenia,walijadili kuhusu walichojifunza kutokana na vurugu za kuondoka Afghanistan baada ya Taliban kukamata nchi, wakati Ujerumani ikipendekeza kwamba wanachama wa EU wabuni kikosi maalum cha wanajeshi 5,000, kitakachoweza kukabiliana na dharura bila kuitegemea Marekani.
Suala hilo limekuwa kwenye ajenda ya EU kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini yalioshuhudiwa Afghanistan hivi karibuni yamepelekea mataifa yote 27 wanachama kulijadili kwa haraka. Mkuu wa sera za mambo ya nje kwenye EU Josep Borrell amesema Alhamisi kwamba anatumai mpango huo utakamilika ifikapo mwezi Novemba. Ameongeza kusema kwamba ni dhahiri sasa kwamba sasa kikosi hicho kinahitajika kwa haraka kufuatia yalioshuhudiwa Afghanistan.
Kuchukuliwa kwa Afghanistan na Taliban pamoja na dharura ya kuokoa maelfu ya watu kwa njia ya ndege baada ya Marekani kuamua kuondoa vikosi vyake nchini humo , kumeonyesha utegemezi mkubwa wa EU kwa Marekani.
Ingawa vikosi vya EU vilikuwa vikisaidiana na Marekani wakati wa kuokoa watu, Marekani kwa sehemu kubwa iisaidia mataifa ya EU kuhamisha watu wake.