Kikosi cha ulinzi wa Mapinduzi ya Iran chakabiliana na wahalifu

Kikosi chenye nguvu cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran kimesambaratisha majambazi wenye silaha kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, televisheni ya taifa imeripoti Jumanne.

Taarifa imesema vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi, vinavyojulikana kama IRGC katika mkoa wa Magharibi mwa Azerbaijan, vilisambaratisha kundi la kihalifu linalopambana na mapinduzi lililokuwa likipanga kuingia Iran kupitia mipaka ya kaskazini magharibi.

Wafuasi kadhaa wa kundi hilo waliuwawa na kujeruhiwa katika operesheni hiyo, na vifaa vyao vilichukuliwa na walinzi, imesema TV ya serikali.

Walinzi walionya hatua yoyote dhidi ya usalama na uthabiti wa eneo la Iran na watakabiliwa na majibu madhubuti.

Ripoti ya televisheni haikufafanua eneo kamili ambalo operesheni hiyo imefanyika.

Mkoa huo una mpaka na nchi mbili, Uturuki na Iraq.