Kikosi cha kijeshi Sudan (RSF) chashambulia kwa  risasi ndege ya Uturuki

wanajeshi wa jeshi la Sudan wakipiga picha katika kituo cha Rapid Support Forces (RSF), tarehe 16, Aprili 2023. Picha na AFP.

Kikosi cha Sudan (RSF) kilishambulia kwa  risasi ndege ya Uturuki ilipokuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Wadi Seyidna nje ya Khartoum siku ya Ijumaa

Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF) kilishambulia kwa risasi ndege ya Uturuki ilipokuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Wadi Seyidna nje ya Khartoum siku ya Ijumaa, na kuharibu mfumo wake wa mafuta, jeshi la Sudan lilisema.

Mamia wamefariki duni na maelfu ya watu wamekimbia katika wiki mbili za mzozo kati ya wapinzani wa kijeshi.

Pande hizo mbili zilikubaliana siku ya Alhamisi kurefusha muda wa usitishaji mapigano kwa saa 72 ili kuruhusu misaada ya kibinadamu, lakini mapigano yalianza tena katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu Khartoum siku ya Ijumaa, kulingana na walioshuhudia na matangazo ya moja kwa moja ya video.