Waziri huyo amefutilia mbali madai kwamba Rusesabagina alitekwa nyara na kupelekwa Rwanda, akisema kwamba nyota huyo wa filamu ya mwaka 1994 kwa jina Hotel Rwanda, iliyoangazia mauaji ya kimbari nchini humo, alipanda ndege na kupelekwa Rwanda bila kushurutishwa na akashuka ndege hiyo mwenyewe.
Rusesabagina, ambaye ni mkosoaji maarufu wa rais wa Rwanda Paul Kagame, anakabiliwa na mashtaka tisa, ikiwemo ugaidi.
Mbunge mmoja wa Marekani Carolyn Maloney alimwandikia barua rais Paul Kagame, kutaka Rusesabagina kuachiliwa huru.
Waziri wa sheria wa Rwanda amesema kwamba mshukiwa amepewa matibabu ya kila mara na wataalam, akifutilia mbali madai madai ya kutopata matibabu.
Anaugua shinikizo la damu na matatizo ya moyo.
Amesema kwamba maafisa kutoka serikali ya Ubelgiji na Marekani wamemtembelea gerezani na kwamba mawakili wake wameruhusiwa kuasiliana naye.