Kesi ya Luigi Mangione aliyemuua CEO wa UnitedHealthcare inaendelea New York

Picha kutoka kitengo cha jela cha Pennsylvania hapo December 10, 2024 ikimuonyesha Luigi Mangione, mshukiwa katika mauaji ya CEO wa UnitedHealthcare huko New York. Pennsylvania December 9, 2024.

Mangione aliondolewa kesi ya awali ya mashtaka ya Pennsylvania kwa mabadilishano na mwendesha mashtaka.

Mshukiwa wa mauaji ya Mkurugenzi Mtendaji wa UnitedHealthcare atarudi New York kujibu mashtaka ya mauaji baada ya kukubali kusafirishwa leo Alhamisi wakati alipofikishwa mahakamani huko Pennsylvania ambako alikamatwa wiki iliyopita baada ya kukimbia kwa siku tano.

Luigi Mangione aliondolewa kesi ya awali juu ya mashtaka ya Pennsylvania katika mabadilishano na mwendesha mashtaka ambapo alimpatia ripoti ya uchunguzi wa kurasa 20 kutoka Idara ya Polisi ya Altoona.

Mangione pia aliondolewa kupelekwa New York. Jaji wa Kaunti ya Blair, David Consiglio aliamuru Mangione akabidhiwe kwa Idara ya Polisi ya New York. Takriban maafisa 12 wa NYPD walikuwa katika chumba cha mahakama.