Kerry awasili Uswizi kwa mazungumzo kuhusu Syria

U.S. Secretary of State John Kerry arrives in Geneva, Switzerland, Sept. 9, 2016.

Huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, akiwasili Uswizi siku ya Ijumaa ili kuanza awamu nyingine ya mazungumzo na mwenzake wa Russia, Sergei Lavrov, maafisa wa kidiplomasia wanaoandamana naye walionekana kutokuwa na matumaini makubwa kuhusu makubaliano yaliyotarajiwa ya kusitisha mapigano nchini Syria.

Afisa mmoja wa Marekani amenukuliwa akisema kuwa hawawezi kutoa hakikisho lolote kwamba makubaliano hayo yatafua dafu.

Lakini Kerry, aliyezungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Russia, Lavrov, takriban mara nne siku ya Jumatano na jana Alhamisi, alikuwa na matumaini na ndiyo sababu alirudi tena Uswizi kwa kile kinachotarajiwa kuwa mkutano usiozidi siku moja.

Kwa siku kadhaa, maswala nyeti yameelezwa nana maafisa wa Marekani kama ya kiufundi. Moja ya maswala hayo, ni kuhakikisha kwamba mji wa Aleppo hautazingirwa tena.