Kere Mwafrika wa kwanza kupata Tuzo ya Usanifu Majengo ya Pritzker

Diebedo Francis Kere (Photo by Odd ANDERSEN / AFP)

Diebedo Francis Kere, mzaliwa wa Burkina Faso, amekuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo ya usanifu majengo, ya Pritz-ker, ambayo ni kubwa zaidi duniani, ya kuwaenzi wachoraji wa nyumba na majengo.

Kere, mwenye umri wa miaka 56, alipokea tuzo ya 51, tangu ilipoanzishwa mwaka 1979, na alionekana mwenye furaha kubwa.

Diebedo Francis Kere, mbunifu na mshindi wa Tuzo ya Pritzker anaeleza: "Sijui habari hii itapokelewaje barani Afrika, lakini kuna jambo moja la uhakika: kwamba tuna vijana wengi wanaotafuta fursa, na kumuona mmoja wao -- ambaye bado ni kijana – akishinda tuzo ya Pritzker, inaweza kufungua nafasi kubwa na ni kielelezo chema kwa ambao wangependa kuwa wasanifu majengo."

Kere, ambaye pia ana uraia wa Ujerumani, anasifika kwa kujenga shule, vituo vya afya, makazi, na majengo mbalimbali, kote Afrika, ikiwa ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Mali, Togo, Kenya, Msumbiji na Sudan.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP