Pia amewataka maafisa wa polisi kujizuilia na kutumia nguvu nyingi na kuwalinda wale wanaofanya maandamano yanayofuata sheria za nchi kwa wale ambao hawajaridhia matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.
Alikuwa akizungumza katika Jumba la Harambee Jumatatu ambapo alikutana na kamati ya maandalizi ya kuingia madarakani.
“Nawaomba wale wote waliopinga matokeo ya uchaguzi kutambua kuwa sote sisi ni Wakenya. Nawaombeni tuendeleze amani na urafiki,” amesema.
“Polisi wako tayari kutoa ulinzi wakati wa maandamano ya amani na wale walioghadhibika watambue hawahitaji ruhsa yangu au ruhsa ya chama cha Jubilee kufanya maandamano ya amani.”
Lakini ametoa onyo kali akisema serikali haitovumilia maisha ya watu kupotea na uharibifu wa mali yanayotokana na uvunjifu wa amani.
Kenyatta amewaonya wale wanaopora na kuharibu mali katika baadhi ya maeneo ya nchi ambako maandamano yaliyofuatia uchaguzi yameripotiwa.
Wakenya wengi wanataka kurejea katika maisha yao ya kawaida baada ya uchaguzi. Hawataki uvunjifu wa amani katika maandamano hayo,” amesema.