Your browser doesn’t support HTML5
Hatua hio imetokana n ongezeko la ajali za barabarani ambapo zaidi ya watu 300 walifariki katika ajali hizo mwezi Disemba pekee.
“Hii leo nataka niseme kuwa maafisa wote wa NTSA waondolewe barabarani kazi ya trafiki iachiwe polisi wa trafiki” asema Uhuru.
Aidha Rais ametaja uendeshaji wa gari kiholela ndiyo unaochangia ajali nyingi zinazoshuhudiwa, huku akitaka kila mmoja anaetumia barabara kuwa muangalifu katika kupunguza ajali za barabarani.
Rais ameyasema hayo katika hotuba yake wakati wa mazishi ya makasisi watatu wa kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa, AIPCA ,waliofariki tarehe 29 Disemba 2017 kutokana na ajali ya barabarani katika barabara kuu ya ya Embu Nairobi.
Watatu hao ni Philip Kubai, Stanley Karuru na Moses Ntoeruri ambao walipata mauti hayo baada ya kutoka mkutano wa maombi , watazikwa katika viwanja vya makanisa wanayohudumu.
Kauli ya rais inajiri baada ya baadhi ya wanasiasa nchini pamoja na mashirika ya asasi za kijamii wakitaka kubanduliwa kwa mamlaka hiyo ya NTSA wakisema kuwa imekua ikitupia lawama washikadau wengine badala ya kutekeleza jukumu lao.
Akinukuliwa na gazeti la tarehe 4 la The star Kenya, Mkurugenzi wa Haki Afrika Hussein Khalid alisema kuwa hatua ya mamlaka hiyo kupiga marufuku safari za usiku imechangia mahangaiko kwa wakenya pamoja na wanafunzi.
Tangu marufuku hiyo itolewe na NTSA , Mamlaka hiyo imekua ikipokea, cheche za maneno kutoka kwa wakenya katika Mtandao wa Twitter, sawia na wabunge,, muungano wa wamiliki wa magari ya uma pamoja na washikadau wengine wa uchukuzi.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Amina Chombo, Kenya