Tangazo hilo lilichapishwa katika toleo maalum la Kenya Gazette la tarehe 21 mwezi Julai mwaka huu.
Jamii hiyo ilikuwa imepeleka ombi rasmi kwa rais la kutaka kutambuliwa kama kabila mnamo mwezi Mei Mwaka huu.
Kaimu waziri wa mambo ya Nnani ya Kenya, Fred Matiang’i, allisifu jamii ya Wahindi nchini Kenya na kusema kuwa imechangia pakubwa katika uimarishaji wa sekta ya elimu na afya.
Hatua hiyo inajiri miezi mitano baada ya jamii ya Wamakonde kutangazwa kama kabila la 43 la Kenya.
Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa baadhi ya wakosoaji wa rais Kenyatta wameitaja hatua hiyo ya kuzifanya jamii hizo kuwa makabila rasmi, kama iliyochochewa na siasa.
Jamii ya Wahindi imekuwa ikiishi nchini Kenya kwa zaidi ya karne moja, na makundi ya kwanza yaliingia nchini mnamo mwisho wa karne ya 18 ili kushiriki katika ujenzi wa reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Wengi wao hawakurudi India baada ya kukamilika kwa ujenzi huo. Wahindi wa Kenya wanafahamika sana kama wenye ustadi wa kufanya aina mbali mbali ya biashara.