Kenya yapata soko la parachichi China

Bidhaa ya parachichi kutoka Mexico imekuwa ikitegemewa sana Marekani. (AP Photo/Armando Solis).

Maparachichi ni chakula kinachopendwa na kawaida hupondwapondwa na kuwekwa kwenye mkate kote duniani, na mahitaji ulimwenguni yanazidi kuongezeka. Hivi sasa wateja wa kichina hatimaye wanaweza kupata ladha ya maparachichi  kutoka Kenya na siyo yale yaliyogandishwa kwenye friji.

Wakati hizi ni habari njema kwa wazalishaji maparachichi nchini Kenya, wachumi wanasema bado hakuna uwiano wa kibiashara.

Wazalishaji avocado wa Kenya wameiambia VOA kuwa wana hamu kubwa kuuza bidhaa yao kwenye nchi hiyo yenye watu wengi sana duniani na wana matumaini kuwa matunda haya, mara nyingine yanaitwa kama ‘dhahabu ya kijani’ yatakuwa na mafanikio kama hilo jina linavyotaja.

Kenya imekuwa ikijaribu kupeleka matunda hayo nchini China bila ya kuyaweka kwenye jokofu, lakini Beijing ilikuwa ikiruhusu matunda yale tu ambayo yamegandishwa kwenye friza ndiyo watayanuaua kwsababu na wasi wasi wa nzi.

Lakini mwezi Agosti, masharti yaliondolewa baada ya wakulima kukidhi vigezo vya ubora.

Chris Flowers, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kilimo Kenya, Kakuzi, alisema Ulaya na Mashariki ya Kati ni masoko mawili makuu ya kampuni hiyo, lakini hivi sasa ana matumaini makubwa kwa soko jingine China.

Flowers anasema “soko la China kwa hakika ni muhimu sana, ni dogo kwa wakati huu ukilinganisha na Ulaya, lakini kuna uwezekano wa kupanuka kwahiyo tuna matumaini kwamba kama tukiendelea kuwa na wateja ndani ya China, litakuwa nalo ni muhimu kama ilivyo muhimu maeneo ya Ulaya.”


Wadau wakuwa wa Kakuzi ni Uingereza, Camelia, alilipa mamilioni ya dola mwaka jana ili kulipa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na Kakuzi. Baadhi ya masoko ya mboga mboga ya Uingereza yalivunja mahusiano nao.


Licha ya shutuma hizo, Kakuzi ilikuwa kampuni ya kwanza ya wakenya kusafirisha avocado fresh kwenda China. Lakini si wazalishaji pekee wa Kenya ambao walianza kusafirisha bidhaa hiyo kwenye taifa hilo kubwa la Asia.

Richard Wafua ni meneja wa Sunripe, kampuni nyingine ambayo imeanza nayo kuiuizia China avocado. Wakati matunda si kawaida kiasili kutumiwa katika upishi wa wachina, anasema avocado zinapata umaarufu mkubwa miongoni mwa wachina.

Wafula anasema “avocado nchini China imekuwa maarufu, na pia wanaagiza kutoka nchi nyingine, na waangalia idadi kubwa ya watu na hivyo mahitaji nayo yatakuwa makubwa.”

Lakini baadhi ya wakenya wanasema ushuru wa asilimia 7 uliowekwa kwa avocado unafanya iwe vigumu kwa Kenya kushindana na avocado kutoka katika nchi nyingine kama vile Mexico na Peru ambako huko hakuna ushuru.

Ubalozi wa China mjini Nairobi haukujibu ombi la VOA kutoa maoni yao.

Hta wakati kuna mkataba mpya wa kuuza nje avocado fresh, Kenya bado inaagiza bidhaa nyingi zaidi kutoka China kuliko zile ambazo wanauza huko. Ukosefu wa uwiano wa kibiashara unaonekana kote katika bara hilo, anasema mchumi wa Kenya, Aly-Khan Satchu. “Kumekuwepo na ukosefu mkubwa wa uwiano wa kibiashara ambao umekuwepo kwa muda mrefu na imekuwa ni kiini cha kutoelewana kati ya bara hilo na China kwa muda hii sasa,” ameongezea Satchu.

Biashara kati ya China na Afrika imefikia kiwango cha juu mwaka jana. China iliuza bidhaa za kiasi cha dola bilioni 148 kwa Afrika mwaka jana na ililipa dola bilioni 106 kwa bidhaa ilizoagiza kutoka katika bara hilo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali huko China.


Rais wa China, Xi Jinping aliapa kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika ili kuleta uwiano wa kibiashara, aliahidi mwaka jana kuongeza uagizaji mpaka dola bilioni 300 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Satchu anasema Afrika ambao kwa kawauda huuza nje ya nchi bidhaa ghafi kwa China, wakati China inauza kila aina ya bidhaa ambazo zimetengenezwa katika bara hilo.

Akijaribu kuzungumzia hili, Rais Xi amekuwa akifanya juhudi za msingi kusukuma na kuingia katika jukwaa la kilimo, Satchu anasema na kuongezea bara lina uwezo mkubwa wa uzalishaji katika kilimo na China ina uhaba wa chakula na hivyo kuna fursa nzuri sana, ambapo nadhani avocado itakuwa ni habari kubwa sana, ambapo tunaweza kutegemea kuwa mauzo makubwa ya nje ya nchi kwenda kwenye soko la China kama njia ya kuzungumzia ukosefu huo wa uwiano.”

Kenya haiweki avocado zake zote katika kikapo kimoja. Pia inazungumza na Malaysia, ili kupanua zaidi soko la avocado duniani.