Kauli ya Matiang'i yajenga taswira mpya Kenya

توضیحات رئیس جمهوری مکزیک، به کامالا هریس معاون رئیس جمهوری آمریکا، در باره آثار دیه‌گو ریورا در کاخ ملی در مکزیکوسیتی

Mara kwa mara serikali ya Kenya imeshtumiwa kwa kutengeneza mazingira duni kukandamiza mashirika ya kijamii yakiwemo yale ya kutetea haki za binadamu, lakini kauli ya serikali iliyotolewa Jumanne inaonyesha kuna mtizamo mpya juu ya uhusiano huo.

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i anasema: "kweli lazima tujifunze kuishi pamoja kama ndugu wamoja ili kuimarisha kazi tunayoifanya; ndugu zetu kutoka mashirika ya kijamii nasema haya kinagaubaga."

Ameongeza kuwa: Msimamo wetu kama serikali ni kuwa mashirika ya kijamii ni mashirika muhimu katika maendeleo ya jamii yetu; ni wenzetu; si raia wa kigeni,tunafurahia kazi wanazofanya,tunakaribisha mtizamo wao na tungependa kushirikiana nao."

Matamshi ya Waziri yanajenga taswira mpya lakini Daisy Amdany, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Community Advocacy and Awareness Trust anaeleza kuwa serikali ina mengi ya kuyafanya kudumisha uhusiano huo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti shutma hizo zimekuwa zikielekezewa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kuratibu utendakazi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Fazul Mohamed.

Bodi hiyo ambayo ni taasisi ya serikali imekuwa ikihisi kuwa mashirika haya yanahujumu utendakazi wa serikali na hivyo basi kutishia kufutilia mbali leseni za baadhi ya mashirika haya.

Wakati Wakenya wakiadhimisha miaka hamsini na mitatu ya Jamhuri mwaka 2016, Rais Uhuru Kenyatta aliyashtumu baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kushirikiana na taasisi fulani za kigeni zinazofadhili mashirika hayo kuhujumu uhuru wa wakenya kuchagua viongozi katika uchaguzi wa mwaka jana.

Na siku mbili baadaye katibu mkuu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho akielekeza jitihada za serikali kuyatambua na kulemaza utendakazi wa baadhi ya mashirika haya yanayotoa hamasisho la elimu kuhusu uchaguzi wa Agosti nane.

Baada ya Rais Kenyatta kutangazwa mshindi wa kura ya Urais katika uchaguzi wa Agosti nane, baadhi ya mashirika haya ya kutetea haki za kibinadamu yalionesha nia ya kupinga ushindi wake katika mahakama ya juu.

Lakini kabla ya kufungua kesi hizo, Bodi inayoongozwa na Fazul Mohamed iliyaagiza baadhi ya mashirika hayo ikiwemo Inuka Kenya, Katiba Institute na MUHURI kufika mbele yake kwa madai kuwa mashirika haya yalihusika kuwaajiri watu wa asili ya kigeni bila vibali miongoni mwa sababu nyingine.

Aidha, Bodi hiyo ilipiga marufuku shughuli za shirika la Kura Yangu Sauti Yangu kwa madai kuwa lilikuwa linafadhili shughuli za kisiasa nchini Kenya.

Harakati hizo zilizidi pale ushindi wa Rais Kenyatta ulibatilishwa, hapa afisi za Shirika la Africog zikifungwa huku usajili wa shirika la Kenya Human Rights Commission ukibatilishwa kwa madai ya kutolipa ushuru.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya.