Mamlaka nchini Kenya zimedhibitisha kuwa mtu aliyeshambulia kituo cha polisi katika eneo la Kapenguria, Kaskazini Mahgharibi mwa Kenya, na kuua maafisa watano, alikuwa ni afisa wa polisi.
Maafisa hao waliuawa mapema Alhamisi na mtu aliyeshambulia kituo hicho na kuanza kupiga risasi kiholela.
Polisi wamesema kuwa mmoja wa waliouawa ni afisa anayesimamia kituo hicho (OCS).
Kamishna wa Kaunti ya Pokot Magharibi Wilson Wanyanga alitoa dhibitisho kwa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kwamba mshambuliaji huyo alikuwa ni afisa wa polisi.
Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari nchini Kenya ilesema kuwa mshambuliaji huyo alimpokonya bunf=duki afisa mmoja na kuanza kufyatua risasi kiholela huku akiwaua watu watano na kuwajeruhi wengine kadhaa.
BMJ Muriithi ana taarifa kamili
Your browser doesn’t support HTML5