Wamesema Jumatano katika taarifa kwamba habari kadhaa zinazochapishwa na wagombea na wafuasi wao katika kambi pinzani za Odinga na Ruto “zilikuwa na lengo la kupotosha wapiga kura na umma juu ya mchakato wa uchaguzi na matokeo ya uchaguzi.
Matokeo ya awali yameonyesha ushindani mkali, lakini idadi ya waliopiga kura ilionekana iko chini kufuatia ongezeko la hasira dhidi ya viongozi wa kisiasa.
Naibu rais William Ruto na mwanasiasa mkongwe wa upinzani Raila Odinga aliyeungwa mkono na chama tawala, wameahidi kudumisha utilivu baada ya zoezi la kupiga kura Jumanne, lakini Wakenya wengi bado wanakumbuka ghasia zilizotokea katika uchaguzi wa miaka iliyopita.
Huku shinikizo likiongezeka kwa tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC) ambayo inatakiwa kutangaza matokeo ifikapo Agosti 16, maafisa wa tume hiyo walifanya kazi usiku kucha kuhesabu kura chini ya uangalizi wa waangalizi.
Mchakato mgumu wa kuhakiki na kujumlisha kura unatarajiwa kuchukua siku kadhaa, na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewataka Wakenya kuwa na subira, na kuepusha madai ya wizi ambayo yalikumba uchaguzi wa awali.