Kenya kuadhimisha mwaka mmoja wa shambulizi la Garissa

Kenya University Attack

Ni mwaka mmoja sasa toka wanamgambo wa Al Shabab wa nchini Somalia kufanya shambulizi baya katika chuo kikuu cha Garissa, nchini Kenya.
Wananchi wa Kenya, wanakumbuka shambulio la kigaidi lililowaua watu takriban 150 mnamo April 2, mwaka jana 2015, tukuo lililoshutumiwa dunia nzima.
Wengi walioangamia wakati huo walikuwa ni wanafunzi wa chuo kikuu wapatao 140, hatua iliyosababisha chuo kikuu cha Garissa kufungwa kwa miazi nane.
Unaweza kusikiliza ripoti ya mwandishi wetu Josephat Kioko wa Mombasa, Kenya alikuwa miongoni mwa waandishi wa kwanza kuripoti habari za njama ya kulipua taasisi za elimu mjini Garissa.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Josephat Kioko kuhusu maadhimisho ya mashambulizi ya Garissa