HABARI KATIKA PICHA: Shambulizi la kigaidi New Zealand

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ataka nchi za magharibi zichukue hatua dhidi ya chuki na ubaguzi dhidi ya Waislam, mjini Gaziantep, Turkey, Machi 15, 2019. baada ya tukio la kigaidi dhidi ya Waislam New Zealand,

Waumini wakiomba dua kwa wahanga na familia zao kutokana na shambulizi la Christchurch wakati wa ibada maalum katika msikiti wa Lakemba, Ijumaa, Machi 15, huko mji wa Wakemba, New South Wales, Australia.

Hisia kutoka nchi mbalimbali ambapo watu wa Pakistani walaani kitendo cha ugaidi dhidi ya Waislam kilichofanyika New Zealand.

Polisi wakilinda eneo la msikiti baada ya tukio la mauaji  huko Linwood, Christchurch, New Zealand, March 15, 2019.

Msikiti mmoja wapo ambapo mauaji yaliyotokea huko nchini New Zealand.

Maafisa wa polisi wakiwa katika harakati za kuwaondoa majeruhi katika eneo la shambulizi la bunduki lililofanywa na gaidi mwenye mrengo wa kulia nchini New Zealand.

Wananchi wa New Zealand wakiwa wanasubiri kupata taarifa za ndugu zao walioathiriwa na shambulizi la kigaidi la mtu mwenye mrengo wa kulia, New Zealand.

Waumini wakihudhuria ibada katika kituo cha utamaduni cha Kiislam New York pakiwa na ulinzi kabambe baada ya tukio la kigaidi dhidi ya Waislam nchini New Zealand Machi 15, 2019.

Dunia imeendelea kulaani shambulizi la mtu mwenye fikra za kigaidi wa mrengo wa kulia lililotokea katika misikiti miwili ya Ijumaa nchini New Zealand.