Kauli mbiu ya mwaka huu, “Ndiyo! Tunaweza kukomesha TB,” inakusudiwa kutuma ujumbe wa matumaini kwamba kukomesha janga hilo, ambalo WHO linasema kila mwaka husababisha vifo vya takriban watu milioni 1.3, kunawezekana.
Wakati ugonjwa huo unatibika na kuzuilika, wakuu wa nchi katika mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu TB wa mwaka 2023 walikadiria kuwa dola bilioni 13 zilihitajika kila mwaka kwa ajili ya kuzuia, utambuzi, matibabu, na matunzo ili kukomesha janga hilo ifikapo mwaka 2030.
Wakuu wa nchi, ambao waliahidi kuharakisha maendeleo ili kukomesha TB na kugeuza ahadi hizi kuwa vitendo vinavyoonekana, waliidhinisha mfululizo wa malengo ya kimataifa ya kusogeza mchakato huu mbele.