Katibu mkuu wa UN yupo Ukraine

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anakutana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guteres hii leo kwa mazungumzo, wakati Ukraine inataka Russia kuwekewa marufuku ya uuzaji wa mafuta yake.

Guteres ameandika ujumbe kwenye Twiter alipofika Ukraine, uliosema kwamba itakuwa vizuri sana vita hivyo vikimaliziak haraka iwezekanavyo, kwa manufaa ya Ukraine, Russia na ulimwengu kwa jumla.

Guterres anajitahidi kuhakikisha kwamba raia wanaondoka katika sehemu zenye mapigano nchini Ukraine na misaada ya kibinadamu inawafikia, ndiyo maswala muhimu yaliyojadiliwa katika kikao na rais wa Russia Vladmir Putin na waziri wa mambo ya nje Sergey Lavrov, mapema wiki hii.

Hayo yakijiri, mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak, amesema Russia itawekewa vikwazo kwa uuzaji wa mafuta katika mda usio kuwa mrefu.

Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya kampuni ya mafuta ya Russia, Gazprom, kusitisha usafirishaji wa mafuta kwenda Poland na Bulgaria. Gazprom ilisema jumatano kwamba Poland na Bulgaria zilikuwa hazijatimiza masharti ya Russia kwamba zilipie mafuta yake kwa kutumia sarafu ya Russia ya rouble.