Modi ametembelea pia hospitali ambapo watu waliojeruhiwa wamelazwa, wakipokea matibabu.
Ripoti ya shirika la habari la Times of India, imesema kwamba moja wapo ya treni iliyohusika katika ajali hiyo ilikuwa ikisafiri kwa njia isiyostahiki, muda mfupi kabla ya ajali kutokea kwa kugongana na treni nyingine.
Serikali ya India imetangaza leo jumamosi kuwa siku ya maombolezi kufuatia ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea Ijumaa usiku, karibu kilomita 220 kusini mwa mji wa Kolkata.
Tarifa ya shirika la habari la The Times of India, inamnukuu mtu aliyeshuhudia ajali hiyo akisema kwamba ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba watu walirushwa nje ya treni kupitia dirishani na milango iliyovunjika.
Miili ya baadhi ya watu ilivunjika miguu na mikono.
Treni tatu zilihusika katika ajali hiyo.