Kardinali Turkson aeleza nia ya kutaka kuondoka kwenye idara muhimu ya Vatican

Kadinali Peter Turkson, wa pili kulia alipokutana na Rais Bashar Al Assad mjini Damascus, Syria, July 22, 2019.

Kadinali Peter Turkson, anayeonekana na baadhi ya watu kama kiongozi ambaye anaweza kuwa mgombea wa nafasi ya kuwa Papa wa kwanza Mwafrika katika takriban miaka 1,500, katika kanisa Katoliki ameeleza ghafla nia ya kutaka kujiuzulu kutoka idara muhimu  ya Vatican

Kadinali Peter Turkson, anayeonekana na baadhi ya watu kama kiongozi ambaye anaweza kuwa mgombea wa nafasi ya kuwa Papa wa kwanza Mwafrika katika takriban miaka 1,500, katika kanisa Katoliki ameeleza ghafla nia ya kutaka kujiuzulu kutoka idara muhimu ya Vatican, vyanzo vinavyofahamu suala hilo vilisema siku ya Jumamosi.

Turkson, mwenye umri wa miaka 73, raia wa Ghana, amekuwa mshauri mkuu wa Papa Francis katika masuala kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na haki za kijamii, na ndiye Mwafrika pekee kuongoza idara ya Vatican.

Kulingana na vyanzo vya habari kutoka Vatican, ambavyo havikutaka kutajwa majina, viliambia shirika la habari la Reuters kwamba Papa bado hajaamua ikiwa atakubali ombi hilo la kujiuzulu.

Turkson anaongoza idara kubwa ya Vatican inayojulikana kama Dicastery for Integral Human Development ambayo iliundwa mwaka 2016 ili kuunganisha ofisi nne zilizokabiliana na maswala kama vile amani, haki, uhamiaji na mashirika ya hisani.