Kanisa moja nchini Afrika Kusini labariki zaidi ya wanandoa 800 siku ya Pasaka

Picha ya mwanaume aliyeoa wake wanne, Afrika Kusini, Septemba 26, 2009.

Zaidi ya wanandoa 800 walifika kanisani Jumapili ya Pasaka katika moja ya sherehe kubwa ya harusi nchini Afrika Kusini tangu mlipuko wa janga la Covid 19.

Kanisa la International Pentecost Holiness linabariki ndoa za wanaume wenye wake wengi, ambazo ni za kawaida katika baadhi ya jamii za Kiafrika, na kanisa hilo linasema kuwa zimeidhinishwa na Biblia.

Misa ya wanandoa wengi hufanyika mara tatu kwa mwaka, siku ya Pasaka, mwezi Disemba na wakati wa maadhimisho ya mwezi Septemba ya kuanzishwa kwa kanisa hilo mwaka 1962.

Lebogile Mamatela, mwenye umri wa miaka 38, ambaye ni mfanyakazi wa serikali ambaye amekuwa mke wa pili kwa baba wa binti yake jana Jumapili, aliiambia Reuters baada ya hafla hiyo: Ni siku isiyo ya kawaida, nina furaha sana. Ninathamini sana wakati huu kwa kuwa miongoni mwa familia ya Mahluku. Ni hisia nzuri.”

Mume wake, Roto Mahluku mwenye umri wa miaka 40, alijiunga na kanisa hilo mwaka 1993 na alimuoa mke wake wa kwanza, Ditopa Mahluku miaka 16 iliyopita. Wana watoto watatu.