Kampuni za China zimeshinda zabuni nne za kuchunguza visima vya mafuta na gesi nchini Iraq, waziri wa mafuta wa Iraq amesema Jumapili wakati nchi hiyo ya Mashariki ya Kati ikiendeleza mzunguko wake wa leseni za gesi ya Hydrocarbon kwa siku ya pili.
Leseni za mafuta na gesi kwa miradi 29 zinalenga kuongeza uzalishaji kwa matumizi ya nyumbani, huku zaidi ya makampuni 20 yakiwa yamepata ufaulu wa awali, yakiwemo makundi kutoka Ulaya, China, Arabuni na Iraq.
Kampuni za China zimekuwa washiriki pekee wa kigeni kushinda zabuni, na kuchukua vitalu tisa vya mafuta na gesi tangu Jumamosi, wakati kampuni ya Kikurdi ya KAR Group ya Iraq ilichukua zabuni mbili.
Hakuna makampuni makubwa ya mafuta ya Marekani, hata baada ya Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia kukutana na wawakilishi wa makampuni ya Marekani katika ziara rasmi nchini Marekani mwezi uliopita.